Jua lachomoza miale,
Nami sitaki nilale,
Toka voi hadi Kitale,
watu mbioni kama mshale,
kutafuta yao Riziki.
Pilkapilka za Maisha,
burura yako rukwama
soma chako Kitabu,
fanikisha lako wazo,
kuelekeza wako ujira,
Pigia dua Rahimu,
hili jambo muhimu,
zaonyesha takwimu,
sitie ulegevu aushini,
ju'mosi siku muhimu.
Makinikeni!